Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 22.09.2021: Martial, Henderson, Kante, Lewandowski, Oyarzabal, Asensio

Pep Guardiola

Chanzo cha picha, Getty Images

Rais wa Barcelona Joan Laporta hajakata tamaa kujaribu kumshawishi bosi wa Manchester City Pep Guardiola arejee Nou Camp.

Guardiola, 50, aliongoza Barca kushinda mataji matatu ya ligi ya Uhispania na Ligi mbili za Mabingwa wakati wa kipindi chake cha miaka minne akiwa usukani kati ya 2008 na 2012(El Nacional - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial atakuwa huru kuondoka Manchester United katika dirisha la usajili la Januari. Mchezaji huyo wa miaka 25 yuko huru kukaa katika Ligi ya Premia lakini anaweza kutafuta fursa barani, na Barcelona inaweza kuwa chaguo (Eurosport)

Mlinda mlango wa Manchester United na England Dean Henderson, 24, anataka uhamisho wa mkopo katika dirisha la uhamisho la Januari. (Sun)

Chelsea wanaandaa ofa mpya za mkataba wa kiungo wa England Mason Mount, 22, kiungo wa Ufaransa N'Golo Kante, 30, na kiungo wa Italia 29, Jorginho. (Standard)

Chelsea walikuwa tayari kutoa euro milioni 100 (pauni milioni 86) kwa ajili ya mlinzi wa Paris St-Germain na mlinzi wa Brazil Marquinhos, 27, katika majira ya joto(RMC Sport - in French)

Chanzo cha picha, Reuters

Mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski anasema "sio lazima ajithibitishe katika ligi nyingine" baada ya kushinda tuzo la mfungaji wa mabao mengi Uropa kwa kufunga mabao 41 ya Bundesliga na Bayern Munich msimu wa 2020-21. (Mirror)

Manchester City wanafuatilia fowadi wa Real Sociedad na Uhispania Mikel Oyarzabal, 24(TeamTalk)

Arsenal itamfanya kipa wa Ujerumani Bernd Leno, 29, apatikane kwa uhamisho kufuatia kuwasili majira ya kiangazi kwa kipa wa Uingereza 23 Ramsdale. (Eurosport)

Barcelona wanajiandaa kuachana na kocha mkuu Ronald Koeman, huku bosi wa Ubelgiji Roberto Martinez akiwa "chaguo bora" kuchukua nafasi ya Mholanzi huyo. (Goal)

Winga wa Uhispania Marco Asensio, 25, anaweza kuondoka Real Madrid ikiwa hatapewa nafasi zaidi za kikosi cha kwanza chini ya Carlo Ancelotti msimu huu(Cadena Ser - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images

Kiungo wa Ureno Joao Palhinha, 26, yuko tayari kupandishwa mshahara huko Sporting Lisbon akihusishwa na kuhamia Everton, Tottenham na Wolves msimu huu wa joto. . (A Bola - in Portuguese)

Kiungo wa kati wa England wa Huddersfield Lewis O'Brien, 22, amekubali masharti ya mkataba mpya na Terriers licha ya ofa nne kutoka kwa Leeds United ya Ligi Kuu. (Football Insider)

Mlinda mlango wa Ajax na Cameroun Andre Onana, 25, anavutia nia kutoka Inter Milan na Napoli(Calciomercato - in Italian)