Mwanaspoti Bora wa Kiafrika wa BBC 2021: Tatjana Schoenmaker
Tatjana Schoenmaker alijiwekea sifa katika mashindano ya mjini Tokyo ambapo hakushinda dhahabu pekee na fedha akiishindia Afrika Kusini , lakini pia aliweka rekodi ya michezo ya olimpiki katika umbali wa mita 200 na mita 100 mtawalia. Kwa kufanya hivyo , aliishindia Afrika Kusini medali ya kwanza katika uogeleaji upande wa akina dada tangu 2000 na kusitisha subra ya taifa lake la miaka 25 ili kupata medali ya upande wa akina dada katika kidimbwi ambapo alimaliza wa kwanza katika fainali ya mita 200.
Schoenmaker karibu ajiondoe mwaka 2016 baada ya kushindwa kufuzu katika michezo ya Olimpiki ya Rio kwa sekunde cha tu. Lakini aliendelea na mchezo huo na kufikia sasa amejishindia mataji kadhaa ya kimataifa na ya kitaifa, medali mbili za dhahabu katika michezo ya Commonwealth Games pamoja na medali ya fedha. Changamoto inayokuja , ni jinsi ya kujiimarisha mimi binafsi? ''nafurahia kuona ni wapi uogeleaji wangu utaelekea'', alisema.