Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 11.12.2021: Ronaldo, Bellingham, Phillips, Fofana, Rudiger, Brereton Diaz, Martial

Cristiano Ronaldo

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha,

Mshambulizi wa Manchester United Cristiano Ronaldo

Real Madrid wanafuatilia hali ya Cristiano Ronaldo katika klabu ya Manchester United. Klabu hiyo ya La Liga inaamini kuwa mkataba wa mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 36 unaweza kusitishwa mwezi Januari kufuatia kuwasili kwa Ralf Rangnick Old Trafford. (Football Insider)

Meneja wa muda wa Manchester United Rangnick ameishauri klabu hiyo kufuatilia kiungo wa kati wa RB Leipzig na Mali Amadou Haidara, 23, kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Muingereza Jude Bellingham, 18, na kiungo wa kati wa Leeds United na England Kalvin Phillips, 26. (ESPN)

Chelsea wanafikiria uwezekano wa kumnunua beki wa Leicester na Ufaransa wa chini ya umri wa miaka 21 Wesley Fofana, 20, huku beki wa Ujerumani Antonio Rudiger, 28, na mchezaji wa kimataifa wa Denmark, Andreas Christensen, 25, wakiwa bado hawajasaini kandarasi mpya Stamford Bridge. (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Beki wa Ujerumani Antonio Rudiger bado hajasaini kandarasi mpya Stamford Bridge

Rudiger anatazamiwa kuwa mmoja wa mabeki wanaolipwa fedha nyingi zaidi katika soka iwapo ataamua kuondoka Chelsea, huku klabu kadhaa za Ulaya zikiwa tayari kumuongezea mara nne mshahara wake wa sasa. (Mail)

Newcastle United, Barcelona, Arsenal na Paris St-Germain wanaongoza katika kinyang'anyiro cha usajili wa mshambuliaji wa Manchester United Mfaransa Anthony Martial,26. (Mirror)

Rais wa Barcelona Joan Laporta anasema klabu inaelekea katika mwelekeo sahihi na kikosi cha kwanza kitaimarishwa katika dirisha la uhamisho la Januari. (Marca)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Newcastle United, Barcelona, Arsenal na Paris St-Germain zinamng'ang'ania mshambuliaji wa Man U Anthony Martial

Barcelona wameongeza dau lao la kumnunua winga Mhispania wa Manchester City Ferran Torres,21, kwa hadi euro miliomi 45 sawa na (£38m) Pamoja na malipo mengine ya ziada ya euro milioni 15 sawa na (£12.8m). (Sport - in Spanish)

Klabu hiyo ya La Liga pia imetathmini uwezekano wa kuwasajili mabeki watatu wa Chelsea kwa uhamisho wa bure. Wachezaji hao ni pamoja na Rudiger, Christensen na Cesar Azpiliceuta, 32 wa Uhispania. (Mirror)

Barca pia wanamnyatia mshambuliaji wa River Plate na Argentina wa miaka 21 Julian Alvarez, ambaye ana kifungu cha kutolewa cha euro milioni 25 swa na (£21.3m). (Sportitalia via AS)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Barcelona wameongeza dau la kumnunua winga wa Manchester City Mhispania Ferran Torres

Kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey anataka kuondoka Juventus ifikapo Januari mwakani, huku Everton na Newcastle zikionesha nia ya kutaka kumnunua mchezaji huyo wa miaka 30. (Gazzetta dello Sport via Football Italia)

Manchester City wanamtaka beki wa Arsenal Mreno Nuno Tavares,21, ambaye alimeonesha uwezo mkubwa uwanjani tangu alipojiung ana klabu hiyo msimu wa joto kutoka Benfica. (ESPN, via Metro)

Arsenal wako tayari kulipa euro milioni 80 (£68m) kumpata mshambuliaji wa Fiorentina's na Serbia Dusan Vlahovic,21. (Sport Mediaset, via Metro)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey kuondoka Juventus ifikapo Januari

Gunners wanakabiliwa na shinikizo la kumuuza kiungo wa kati Muingereza Ainsley Maitland-Niles, 24, ambaye anazidi kuchanganyikiwa kwa kukosa muda wa kucheza. (Mail)