Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Origi, Pulisic, Bereton Diaz, Phillips, Dembele, Danjuma, Cook

Divock Origi

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa Liverpool na Ubelgiji Divock Origi, 26, analengwa na klabu ya Serie A.AC Milan - ambayo inatafuta wachezaji walio tayari kuchukua nafasi ya Zlatan Ibrahimovic - na Atalanta. (Tutto Mercato)

Tottenham wameanza mazungumzo ya kandarasi na mlinda mlango wa Ufaransa na nahodha wa klabu hiyo Hugo Lloris, 34, kabla ya mkataba wake wa sasa kukamilika msimu ujao wa joto. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona ina mpango wa kuwasajili wachezaji watatu wa Chelsea akiwemo winga wa Marekani Christian Pulisic 23, Beki wa Ujerumani Antonio Rudiger 28, na beki Cesar Azpilicueta, 32. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Leeds bado wana hamu ya kumnunua mshambuliaji wa Chile Ben Brereton Diaz, 22, licha ya Blackburn kuweka bei ya pauni milioni 25 ili kumnasa. (Sun)

West Ham wanamlenga mlinzi wa Uingereza Nat Phillips, 24, kama mbadala wa Muitaliano aliyejeruhiwa Angelo Ogbonna, 33, lakini Liverpool wanadai pauni milioni 10 ili kumwachilia.(Sun)

Chanzo cha picha, Reuters

Winga wa Bayern Munich Mfaransa Kingsley Coman, 25, anasitasita kusaini kandarasi mpya katika uwanja wa Allianz Arena, na ikiwa hatafanya hivyo, mchezaji mwenzake wa kimataifa Ousmane Dembele, 24, ambaye anakaribia mwisho wa mkataba wake Barcelona, ana uwezekano mkubwa wa kuwa mbadala.(Christian Falk)

Real Madrid hawana mpango wa kumuuza mshambuliaji wa Brazil Rodrygo, 20, licha ya kuhusishwa na Liverpool. (Fabrizio Romano)

Lyon pia wanataka kumsajili winga wa Villarreal Mholanzi Arnaut Danjuma, 24. Manchester United na Barcelona pia wanaaminika kufuatilia maendeleo yake.(TodoFichajes-in Spanish)

Newcastle wataelekeza mawazo yao kwa mlinzi wa Bournemouth Muingereza Steve Cook, 30, baada ya kupunguzwa bei ya kumnunua beki wa kati wa Burnley James Tarkowski, 29. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Mlinzi wa Manchester United na Ureno Diogo Dalot, 22, alikuwa akilengwa na Roma na mkufunzi wa zamani Jose Mourinho lakini mechi zake za hivi majuzi chini ya mkufunzi mpya wa Reds Ralf Rangnick zinafanya kushindwa kuhama, kumaanisha kuwa klabu hiyo ya Serie A inatafuta mbadala ikiwa ni pamoja na mchezaji anayekipiga Norwich ,Muingereza Max Aaron, 21, n Benjamin Henrichs wa RB Leipzig na Ujerumani, 24.(Corriere Dello Sport)

Mlinzi wa Arsenal na Ufaransa William Saliba, 20, amesema "angependelea kutozungumza" kuhusu mustakabali wake kwa kuhamia klabu ya Ligue 1 ya Marseille. (RTL,via Mirror)

Arsenal wanatatizika kumbakisha mshambuliaji Muingereza Khayon Edwards, 18, ambaye tayari ameshafunga mabao 14 msimu huu na amebakiza miezi sita pekee katika mkataba wake. Chelsea, Leeds, Southampton, Brighton na Newcastle zote zinafuatilia maendeleo, pamoja na vilabu vingi nchini Ujerumani.(Mail)