Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Cavani, Rudiger, Alli, Botman, Lingard, Diaz

Edinson cavani

Chanzo cha picha, Getty Images

Kaka wa Edinson Cavani ameashiria kuwa mshambuliaji huyo anakaribia kuondoka Manchester United, huku kukiwa na uwezekano wa kuhamia Brazil. (Manchester Evening News)

Manchester United wako tayari kushindana na wapinzani wa ligi ya primia, Liverpool na Manchester City katika kumsaka winga wa Porto Luis Diaz, 24.(Fichajes, via Team Talk)

Chanzo cha picha, Getty Images

Real Madrid wameibuka kuwa wanaopendelewa katika kumsajili mlinzi wa Chelsea Antonio Rudiger baada ya mazungumzo mazuri na Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 28 kuhusu kujiunga nao bila malipo msimu ujao wa joto.(Guardian)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maisha ya Kiungo wa kati Dele Alli akiwa Tottenham huenda yakafikia kikomo kwani kocha mpya Antonio Conte hamuoni mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 katika mipango yake.(The Athletic, via Star)

Newcastle wamemfanya mlinzi wa kati wa Lille Sven Botman, 21, kuwa usajili wa kipaumbele katika dirisha la uhamisho la Januari huku winga wa Manchester United Jesse Lingard, 28, pia akiwa kwenye orodha ya Eddie Howe.(Guardian)

Barcelona, ​​Juventus na klabu ya Corinthians ya Brazil wana nia ya kumsajili Cavani wa Manchester United.(Marca)

Manchester United wako tayari kushindana na wapinzani wa ligi ya primia, Liverpool na Manchester City katika kumsaka winga wa Porto Luis Diaz, 24.(Fichajes, via Team Talk)

Kocha wa Burnley Sean Dyche anasema klabu hiyo haitatumia kiasi kikubwa katika dirisha la uhamisho la Januari.(Talksport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji aliyesahaulika wa Aston Villa Keinan Davis, 23, ameibuka kama shabaha ya uhamisho wa Januari na klabu inayoshiriki ligi daraja la kwanza Nottingham Forest.(Birmingham Live)

Brentford wamewasiliana na Braga kuhusu uwezekano wa kumnunua beki wa kushoto wa Ureno Francisco Moura, 22 Januari.(Sun)