Ligi ya primia iliripoti visa 42 vya covid 19 wiki iliyopita

Chanzo cha picha, Getty Images
Wachezaji 42 wa Ligi ya Primia na wafanyakazi walikutwa na covid 19 wiki iliyopita - vikiwa ndivyo visa vingi zaidi kurekodiwa kwenye Ligi katika kipindi cha siku saba.
Ndiyo idadi ya juu zaidi tangu visa 40 vilivyoripotiwa mwezi Januari.
Wakati huo vipimo 2.295 vilifanywa huku vipimo 3,805 vikifanyaa hivi majuzi kati ya tarehe 6 na 12 mwezi huu wa Desemba.
Brighton, Tottenham, Leicester, Manchester United, Aston Villa na Norwich wote wamethibitisha visa huku mechi kati ya United na Brentford ikihairishwa.
Mechi ya Jumapili kati ya Brighton na Tottenham pia ilihairishwa kufuatia mlipuko wa covid 19 huko Spurs.
Idadi ya juu zaiidi ya visa vya covid 19 vilikuwa ni 16 kati ya tarehe 16 na 22 mwezi Agosti ambapo vipimo 3,060 vilifanywa.
Alhamisi kufuatia kutangazwa sheria mpya za kukabiliana na covid 19 nchini Uingereza Ligi ya Primia iliwaambia vilabu virejee kwenye huduma za dharura ikiwemo kukaa umbalia na wenzao na kuvaa barakoa
Kuanzia Jumatano mashabiki watahitajika kuonyesha ushahidi wa kuchanjwa mara mbili au matokeo ya vipimo kuonyesha hawana virusi ili kuhudhuria mechi huku mashabiki 10,000 wakiruhusiwa nchini Uingereza, Hii ni pamoja na kwa mechi za Ligi ya Primia.
Ni vilabu vipi vya Primia vinakumbwa na milipiko ya covid 19?
Mechi kati ya Tottenham na Rennes ilihairishwa Alhamisi kwa sababu ya mlipuko iliyochangia kuharishwa kuhairishwa mechi ya Brighton.
Pia Alhamisi wachezaji kadhaa wa Leicester hawakusafiri kwenda Italia kwa mechi yao ya Europa dhidi ya Napoli kutokana na kugunduliwa visa vya covid 19.
Jumatatu Ligi ya Primia ilithibitisha kuwa mechi kati ya United na Brentford ilihairishwa.
Meneja wa Aston Villa Steven Gerrard alithibitisha kuwa wafanyakazia kadhaa na wachezaji walikuwa na covid 19 lakini akasisitiza kuwa wengine wengi walikuwa salama.
Kocha mkuu wa Brighton Graham Potter anasema kuwa kuna visa vitatu au vinne vya covid
Mameneja wanasema nini kuhusu covid 19?
Chanzo cha picha, Getty Images
Kabla ya kuhairishwa meneja wa Brentford Thomas Frank aliunga mkono wito wa meneja wa Arsenal Mikel Arteta wa kutaka kutangazwa ratiba iliyo wazi kutoka Ligi ya Primia kuhusu mabadiliko yaliyosababishwa na visa vya covid 19.
Meneja wa Machester City Pep Guardiola alisema anawashauri wachezaji wake kupata chanjo nyingine: Tunazungumza na wachezaji kila siku kusema chukua tahadhari, Linda afya, vaa barakoa na kaa mbali na wengine.
Meneja wa Burnley Sean Dyche alifichua kuwa hawezi kuwahubiria wachezaji kuhusu chanjo.
Sheria kwa mashabiki ni zipi kwenye mechi za Ligi ya Primia?
Hatua ya serikali ya kutangza mpango wa pili siku ya Jumatano kupambana na kusambaa kwa kirusi cha omicron yamaanisha itakuwa ni lazima kwa mashabiki kuonyesha ushahidi wa kuchanjwa mara mbili au vipimo ili kuweza kuhudhuria mechi huku watu 10,000 wakiruhusiwa kuhudhuria nchini Uingereza.
Vilabu vya Primia vimefanya ukaguzi kwa mashabiki msimu huu ambapo Brighton, Chelsea na Tottenham vikiwa miongoni kwa wale wanahitaji kuwa na vyeti vyai kuingia.
Brighton wanacheza na Wolves siku ya Jumatano na mkurugenzi wa Seagulls Paul Narber alisema na matumaini kuwa iwapo mashabiki watafuata sheria mpya hakutakuwa na vizuizi kwa idadi ya mashabiki ambao watahuduria.
Barber alisema mashabiki wa Brighton watahitajika kujaza fomu za mitandaoni na wavae barokoa ndani ya uwanja