Tatjana Schoenmaker: Mafanikio ya Olimpiki bado 'yanahisi si ya kweli' kwa Muafrika Kusini

  • By Rob Stevens
  • BBC Sport Africa
Tatjana Schoenmaker akishangilia medali yake ya dhahabu katika Olimpiki ya Tokyo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Tatjana Schoenmaker alishinda medali ya kwanza ya dhahabu ya Olimpiki ya Afrika Kusini katika uogelea upande wa kinadada tangu 1996.

Licha ya imani thabiti ya Tatjana Schoenmaker, muogeleaji huyo wa Afrika Kusini amepata ugumu kuamini mafanikio yake mwaka huu kwa kiasi fulani baada ya kurejea kutoka Olimpiki ya Tokyo akiwa na medali mbili na rekodi moja ya dunia.

Mafanikio yake mengi yalikuja miaka mitano baada ya kukosa kushiriki Michezo ya Rio, baada ya kushindwa kufuzu kwa mia moja tu ya sekunde, hivyo kufanya mafanikio yote kuwa matamu.

Ushindi wake wa mita 200 2 breaststroke ulithibitika kuwa ni medali pekee ya dhahabu ya Afrika Kusini nchini Japani, na ilikuwa ni medali ya kwanza ya mwanamke nchini mwake katika Olimpiki tangu bingwa Penny Heyns alipotwaa shaba mwaka wa 2000.

"Kwa kweli bado inahisi kuwa sio kweli," Schoenmaker, 24, aliiambia BBC Sport Africa.

"Unaota kama msichana mdogo kuafikia kitu cha kiopekee kwenye Olimpiki, lakini sidhani kama unaamini kinaweza kutokea.

"Inahisi kama ndoto. Unafanya kazi kwa miaka 16 kufika huko na wakati uliisha haraka sana. inahisi kama jambo la ajabu."

"Nilipotazama bodi mara ya pili, ndipo nilipogundua - 'subiri, nimevunja rekodi ya dunia'," alikumbuka.

"Mtazamo wangu wa kwanza ulikuwa mbaya sana kwa mtu ambaye angeshinda na kuvunja rekodi ya dunia, lakini kwa hakika nilifanikiwa kwa majibu hayo ya pili."

Machozi zaidi yalifuata katika sherehe ya medali.

"Kocha wangu ananitania na kusema nahitaji kupata mfadhili wa tishu," alisema.

"Si mara zote mashindano yanapendeza kwa sababu yanaumiza na kuna hofu. Lakini angalau unapokuwa [jukwaani], kila kitu kinawekwa kando na ni wewe tu kuzingatia kuimba wimbo huo na kuweka bendera ya nchi yako juu. unapoimba wimbo wako wa taifa, unajivunia sana."

Msukumo wa kidini kupitia changamoto

Maelezo ya video,

Tatjana Schoenmaker: Muogeleaji wa Afrika Kusini

Kuogelea hakujawa jambo la kwa moja kwa Schoenmaker, ambaye alikaribia sana kuacha mchezo huo mwaka wa 2016 baada ya kushindwa kufuzu kwa mashindano ya Rio.

Aliacha kufurahia mchezo huo lakini akareja kwa mtindo wa kuvutia, akisajilirekodi nyingi za kitaifa na bara, mataji mawili ya Michezo ya Jumuiya ya Madola mnamo 2018 na medali ya fedha ya Mashindano ya Dunia ya 2019.

Leo, anakubali changamoto zilimnufaisha.

"Naangalia nyuma nilivyokuwa - kijana wa miaka 19, sikuwa na uzoefu hata kidogo - na labda haikuwa bora kwangu kwenda [Rio]," anasema.

"Tabia yangu ilibidi ijengeke. Na kwa hivyo nikitazama nyuma, sijutii hilo. Inakufanya utambue kwamba Mungu kweli ana mpango kwa kila mtu."

Imani ya ucha mungu ya Schoenmaker ndiyo inayomsukuma.

"Nilibarikiwa na talanta ya kushangaza," alisema. "Na ninataka kutumia talanta hii ambayo Mungu alinipa kujaribu na kulitukuza jina lake, ili kunitia moyo kila siku."

Kujitolea kwake ni kwa nguvu sana hivi kwamba tofauti na wengine wanaojishughulisha na sauti za muziki , yeye hufanya hivyo kwa kusikiliza injili.

"Ninajua watu wanataka kusikiliza muziki - kama wa Eminem - lakini mimi huzingatia sana ninaposikiliza muziki wa kuabudu," anaelezea. "Pia inakukumbusha unafanya hivyo kwa ajili ya nani."

'Imani ndani yangu ilikuwepo'

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Schoenmaker alijawa na hisia baada ya kushinda fainali ya Olimpiki ya mita 200 ya breaststroke katika muda wa rekodi ya dunia.

Schoenmaker aliweka rekodi ya Olimpiki katika mashindano yake ya kwanza mjini Tokyo, akitumia saa 1:04.82 katika raundi yake ya mita 100, jambo ambalo lilimruhusu "kuvunja barafu" na kuogelea kwa uhuru kamili kuanzia hapo na kuendelea.

Hatimaye alichukua medali ya fedha kwa umbali mfupi zaidi, na uzoefu wake kuweka msingi kwa ajili ya mafanikio yake ya mita 200 siku tatu baadaye.

"Kwa fainali yangu ya 100, nililenga sana kujaribu kubaki mbele ya mshikilizi wa rekodi ya dunia [Lilly King] hivi kwamba sikumwona msichana karibu nami."

Ni maumbile ya asili ya Kikristo ya Schoenmaker kwamba anaonekana kufurahishwa sana na Mmarekani Lydia Jacobs, mwenye umri wa miaka 17 ambaye alinyakua dhahabu.

"Nilimfurahia sana - zilikuwa mbio za ajabu sana. Niliingia pale [nafasi] ya saba au ya nane kwa hivyo kuondoka na medali hakika haikuwa kile nilichofikiria ningefanya.

"Nikiingia kwenye mbio za mita 200, niliweza kuogelea tu mbio zangu. Sikuwa na chochote cha kuthibitisha kwa mtu yeyote au mimi mwenyewe kwa sababu nilijua kuwa naweza kufanya vyema. Imani yangu kwangu ilikuwa pale."

Schoenmaker sasa anatumai kuwapa wengine imani baada ya kuunda wakfu wa kutoa fedha kwa Waafrika Kusini ambao hawawezi kuogelea lakini pia wale wanaofanya vizuri.

"Kama ningeweza kumsaidia mtu kupata ujuzi huo wa kimsingi wa kuogelea, hasa wale ambao hawana uwezo wa kumudu, hilo litakuwa jambo zuri, hasa kwa sababu tuna matatizo mengi ya kuzama majini kwa watu katika maeneo ya mijini," alisema.

Pia anataka kuwasaidia wale wanaoota kumwiga katika siku zijazo.

"Wakati mwingine ukichaguliwa kwa ajili ya mashindano ya dunia, unapaswa kulipa kiasi kikubwa cha fedha na watu wengi hawawezi - hivyo basi wanaacha ndoto hiyo kwa sababu hawawezi kulipa," anasema.

"Ningewasaidia kifedha kupata uzoefu hata kidogo wa yale niliyopitia."

Mwanadada anayejitambua - ambaye anaifurahia "sio kwa medali na rekodi, lakini kupenda tu kuifanya kila siku" - Wakati mzuri wa Schoenmaker wa 2021 unatoa heshima kwa safari yake wakati wa mzunguko wa mwisho wa Olimpiki.

"Jambo la kuangazia ni kuona tu jinsi ulivyokua kibinafsi na kiroho. Changamoto inayofuata ni: ninawezaje kujiboresha? Ninafurahi kuona mahali ambapo kuogelea kwangu kutaenda."

Tafadhali Mpigie kura Mwanamichezo Bora wa Afrika wa BBC 2021 ambapo pia utapata sheria na ilani ya faragha. Upigaji kura utafungwa Jumapili Disemba 19 2021 saa 23:59 GMT."

Mahojiano na Tatjana Schoenmaker na Victoire Eyoum.