Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 15.12.2021: Alli, Pogba, Martial, Lingard, Milenkovic, Vlahovic, Castellanos

Chanzo cha picha, Empics
Anthorny Martial
Atletico Madrid wanataka kutazama uwezekano wa kufanya makubaliano na Manchester United kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 26. (Eurosport)
West Ham inajiandaa kusonga mbele kwa kutaka kumnunua Nat Phillips wa Liverpool mwezi Januari, licha ya jeraha la hivi majuzi la beki huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24. (Standard)
Chanzo cha picha, Reuters
Newcastle wamefanya ufuatiliaji wa awali kuhusu Dele Alli, huku Tottenham wakiwa tayari kusikiliza ofa kwa kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 25. (Teamtalk)
Manchester United wanaangalia walengwa wa safu ya kiungo huku Paul Pogba, 28, akitarajiwa kuondoka bure wakati mkataba wa kiungo huyo wa kati wa Ufaransa utakapokamilika msimu wa joto.(Telegraph)
United haitarajii Jesse Lingard kuondoka katika dirisha la uhamisho la Januari huku kiungo huyo wa kati wa Uingereza mwenye umri wa miaka 28 akikaribia miezi sita ya mwisho ya mkataba wake.(Manchester Evening News)
West Ham pia wana matumaini ya kumnunua Nikola Milenkovic kama makubaliano kati ya mlinzi huyo wa Serbia mwenye umri wa miaka 24 na mmiliki wa Fiorentina yanamaanisha kuwa huenda akahama.(Teamtalk)
Chanzo cha picha, Getty Images
Fiorentina wameweka bei ya euro milioni 100 (£85m) kwa mshambuliaji wao wa Serbia Dusan Vlahovic, 21.(Gazzetta Sport)
West Ham inamfuatilia mshambuliaji wa Argentina wa New York City Valentin Castellanos, 23.(Mail)
Paris St-Germain, Barcelona, Liverpool, Manchester City na Tottenham wote wanafikiriwa kumfuatilia mlinzi wa kushoto wa Ufaransa Rayan Ait-Nouri, 20, lakini Wolves watapokea 50% pekee ya ada yoyote ya uhamisho kutokana na kifungu cha mauzo.(Mail)
Kocha wa Sheffield Wednesday Darren Moore amethibitisha kuwa klabu hiyo iko kwenye mazungumzo na Everton ili kuamua kama mlinzi wa Uingereza Lewis Gibson, 21 anafaa kuendelea na kipindi chake cha mkopo huko Hillsborough mara tu atakapopona jeraha.(Liverpool Echo)
Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona wanapanga mpango wa kumnunua beki wa kushoto wa Chelsea Mholanzi Ian Maatsen, 19, ambaye yuko kwa mkopo wa msimu mzima na klabu ya Championship Coventry.(Football Insider)
Leicester City wanavutiwa na mshambuliaji wa Swansea Mholanzi Joel Piroe, 22. (Swansea independent)