Hutton apunguziwa adhabu

Beki wa Sunderland Alan Hutton amepunguziwa adhabu yake ya kutocheza mechu tatu.

Hutton sasa atakosa mechi moja, kufuatia kuoneshwa kadi nyekudu kwenye mchezo dhidi ya Hull ambapo waliichapa timu hiyo kwa bao 1-0.

Chama cha soka cha England, FA, kimepunguza adhabu hiyo kufuatia rufaa iliyokatwa na Sunderland.

Hutton alimtupia mpira Jozy Altidore, aliyeghadhibika na kitendo hicho na kumpiga kichwa beki huyo aliyelazimika kupatiwa matibabu.

Mwamuzi Lee Robert aliwaonesha kadi nyekundu wachezaji wote wawili.