Murray atolewa na Ferrer

Andy Murray
Image caption Murray amekula kichapo kutoka kwa Ferrer

Andy Murray ameng'olewa kwenye michuano ya Rome Masters na David Ferrer katika raundi ya tatu ya michuano hiyo.

Murray ambaye ni namba tano duniani alijitutumua kuepuka kutolewa katika michuano ya ATP siku ya Alhamisi, baada ya kupata ushindi wa seti 6-2 6-4, dhidi ya Andreas Seppi.

Hata hivyo Murray alishindwa kutamba na kuchukua pointi muhimu wakati akicheza na Ferrer kwa kupoteza service moja katika kila seti.

Wakati huohuo, bingwa namba mbili duniani Novak Djokovic amesonga mbele katika michuano hiyo na kutinga robo fainali kwa kumshinda Thomaz Bellucci kwa pointi 6-4 6-4.

Djokovic atapambana na Fernando Verdasco. Verdasco alimtoa Guillermo Garcia-Lopez kwa seti 6-4 7-6 (7-2).