Neville atia saini mkataba mpya United

Nahodha wa Manchester United Gary Neville ametia saini mkataba wa mwaka mmoja na Manchester United.

Image caption Nahodha wa United, Gary Neville

Neville mwenye umri wa miaka 35, hakucheza mechi kwa karibu miezi 18 kufuatia kutenguka kiwiko cha mguu mwezi machi 2007.

Hata hivyo ameweza kucheza mechi 27 msimu huu. Amecheza karibu mara 600 tangu mechi yake ya kwanza kwa United mwaka 1992.

Image caption Gary Neville akimpongeza mkongwe mwenzake Paul Scholes

Beki huyo wa upande wa kulia, anaungana na wakongwe wengine Paul Scholes na Ryan Giggs walioongeza mikataba yao Old Trafford.

Kuingia kwa Rafael Da Silva kumesababisha Neville kukosa baadhi ya mechi na kijana huyo kutoka Brazil kupata nafasi ya kucheza.