United yaichapa Sunderland

Chelsea watalazimika kusubiri hadi siku ya mwisho ili kuanza kusherekea ushindi wa ligi kuu ya England baada ya Manchester United kuishinda Sunderland kwa bao 1-0.

Image caption Bao pekee limefungwa na Nani

Chelsea italazimika pia kushinda mchezo wake dhidi ya Wigan siku ya mwisho ili kushinda ligi hiyo.

United imepata ushindi dhidi ya Sunderland kwa bao pekee lililofungwa na Nani katika dakika ya 28.

Chelsea sasa imefikisha pointi 83, huku United wakiwa na pointi 82. Man United watacheza na Stoke City katika mchezo wake wa mwisho.