Fulham yakataliwa kubadilisha mechi

Klabu ya Fulham imegonga mwamba kufuatia maombo yake ya kutaka mchezo wa kumalizia msimu wa Ligi Kuu ya England siku ya Jumapili uchezwe Jumamosi.

Image caption Gera akishangilia bao lililoipeleka fainali Fulham ya Europa

Fulham walitaka kuikabili Arsenal mapema kidogo ili waweze kupata muda wa kutosha kujiandaa kwa mechi ya fainali ya Ligi ya Europa dhdi ya Atletico Madrid.

Fulham itacheza mjini Hamburg siku ya Jumatano, lakini Bodi ya Ligi Kuu ya England inataka kuhakikisha kunakuwa na uadilifu katika mashindano ya nyumbani.

Wakati huo huo, Fulham imeiomba Uefa tikiti zaidi kwa ajili ya mchezo wa fainali baada ya kuuza mgao wa tikiti zake zote 12,650.

Fulham imedai upungufu wa tikiti kwa ajili ya mechi dhidi ya Atletico Madrid umetokana na "mahitaji ya kupindukia," baada ya kuuza tikiti zote katika muda wa saa nne.

Lakini kundi la mashabiki wa Fulham wamelaumu uamuzi wa kuwaruhusu wale wenye tikiti za msimu kuuziwa hadi tikiti nne kwa mchezo mmoja.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa mawasiliano wa Fulham Sarah Brookes "Tunaendelea kuwashawishi wahusika tupatiwe tikiti zaidi, mashabiki ni lazima wajisajili kwetu."

Uefa, Shirikisho linalosimamia soka barani Ulaya, halikuweza kusema chochote juu ya maombi ya Fulaham kwa ajili ya kupatiwa tikiti zaidi kwa mchezo wa Jumatano.

Klabu hiyo ya Craven Cottage inao mashabiki wenye tikiti za msimu 10,000 lakini uamuazi wa kuwaruhusu kununua tikiti hadi nne kwa mtu mmoja inaama mashabiki wengine wa kawaida wamezikosa.

Tikiti ziliuzwa siku ya Ijumaa saa moja asubuhi, chini ya saa kumi na mbili baada ya Fulham kufanikiwa kufuzu kucheza hatua ya fainali kwa mara ya kwanza katika michuano ya Ulaya baada ya kuwalaza hamburg mabao 2-1.