Hispania yataja kikosi

Wachezaji watatu majeruhi Cesc Fabregas, Fernando Torres na Andres Iniesta wameteuliwa katika kikosi cha awali cha Hispania cha Kombe la Dunia.

Image caption Torres

Fabregas amevunjika mfupa wa mguu, Torres amefanyiwa upasuaji wa goti akiwa anapona vizuri kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Hispania.

Kiungo wa Barcelona Iniesta naye ana matatizo ya mguu akitarajiwa kupona wakati wa fainali za Kombe la Dunia.

Kocha wa Hispania Vincente del Bosque, atakayepunguza kikosi chake na kubakiwa na wachezaji 23 hadi itakapofika tarehe 1 Juni, amewaita walinda mlango ambao awali hawakuchezea timu ya taifa Victor Valdes na David De Gea pamoja na mshambuliaji Pedro.

Kikosi cha Hispania

Walinda Mlango: Iker Casillas (Real Madrid), David De Gea (Atletico de Madrid), Diego Lopez (Villareal), Jose Manuel 'Pepe' Reina (Liverpool), Victor Valdes (Barcelona).

Walinzi: Raul Albiol (Real Madrid), Alvaro Arbeloa (Real Madrid), Cesar Azpilicueta (Osasuna), Joan Capdevila (Villarreal), Carlos Marchena (Valencia), Gerard Pique (Barcelona), Carles Puyol (Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid).

Wachezaji wa Kiungo: Xabier Alonso (Real Madrid), Sergio Busquets (Barcelona), Cesc Fabregas (Arsenal), Andres Iniesta (Barcelona), Javier Martinez (Athletic Bilbao), Marcos Senna (Villarreal), David Silva (Valencia), Xavi Hernandez (Barcelona).

Washambuliaji: Santiago Cazorla (Villarreal), Jesus Navas (Sevilla), Juan Manuel Mata (Valencia), Pedro Rodriguez (Barcelona), Daniel Guiza (Fenerbache), Fernando Llorente (Athletic Bilbao), Alvaro Negredo (Sevilla), Fernando Torres (Liverpool), David Villa (Valencia).