4 Juni, 2010 - Imetolewa 17:27 GMT

Picha: Unashabikia timu gani?

Msisimko wa Kombe la Dunia 2010

 • Vijana wakisakata kabumbu huko Maridi nchini Niger.
  Vijana wakisakata kabumbu huko Maridi nchini Niger. [Picha na Tchima Illa Isoufou/BBC]
 • Mashabiki wa The Elephants walipokuwa wakishangilia ushindi mwingine dhidi ya Burkina Faso katika eneo la Blockoss, mjini Abidjan. [Picha na John James/BBC]
 • Kiungo nyoya wa Ghana, Michael Essien, ingawa hatacheza Afrika Kusini, lakini ana mashabiki lukuki nchini Kenya kama inavyoonekana nyuma ya basi hili. [Picha na Peter Njoroge/BBC]
 • Nyota wa baadaye: Huenda Drogba, Rooney na Messi wapya wakatoka katika mojawapo ya vijana hawa waliokutwa wakisakata kabumbu Kibera mji mkuu Nairobi nchini Kenya. [Picha na Peter Musembi/BBC]
 • Samuel Eto'o anatamba katika matangazo ya biashara mjini Nairobi. [Picha na Peter Njoroge/BBC].
 • Kumbukumbu kutoka picha maalum ya The Leopards, iliyokuwa Zaire, sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakati waliposhiriki fainali za mwaka 1974, ilipokuwa timu ya kwanza kutoka kusini mwa jangwa la Sahara. [Picha na Peter Musembi/BBC].
 • Mashabiki wa Ivory Coast walipokuwa katika uwanja wa Felix Houphouet-Boigny ambapo Guinea ilitandikwa. [Picha na John James/BBC].
 • Mfanyabiashara akinadi vifaa vya michezo, hasa mipira na viatu nje ya uwanja wa City mjini Nairobi. [Picha na Peter Njoroge/BBC].
 • Soka si mchezo maarufu nchini Ethiopia kama inavyoonekana kwenye uwanja huu mtupu, licha ya kuwa hii ni mechi muhimu ya ligi kuu ya Ethiopia. [Picha na Peter Musembi/BBC].
 • Mwanamke akipita mbele ya uwanja wa Nyayo mjini Nairobi katika siku kulipokuwa na mechi lakini hakuna mashabiki. [Picha na Peter Musembi/BBC].
 • Na mwisho kabisa, wanafunzi watatu wakipiga picha mwisho wa mazoezi ya soka kwenye chuo huko Enugu, Nigeria. Tunakaribisha picha za kila aina kuhusu kombe la dunia, tutumie kupitia: yourpics@bbc.co.uk. [Picha na Abdulsalam Ibrahim Ahmed/BBC].

BBC navigation

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.