16 Juni, 2010 - Imetolewa 20:35 GMT

Afrika Kusini yanyukwa na Uruguay

Matumaini ya Afrika Kusini kufanya vyema katika mashindano ya Kombe la Dunia yanayofanyika katika ardhi yake, yamefifia baada ya kufungwa 2-0 na Uruguay katika mechi iliyochezwa uwanja wa Loftus Versfeld mjini TShwane au Pretoria.

Afrika Kusini walianza kwa gonga zilizowapatia sare kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya Mexico, lakini kadri muda ulivyokuwa ukisonga mbele, walianza kumeguka na kushindwa kuhimili vishindo na njama za washambuliaji wa Uruguay.

Kunako dakika ya 24, Diego Forlan aliachia mkwaju wa mbali ambao ulienda kushoto kwa mlinda mlango Itumeleng Khune ambaye hata hakuweza kuruka kujaribu kuufikia.

Alikuwa ni mlinda mlango Itumeleng Khune, aliyebadilisha taswira ya matumani ni ya Afrika Kusini wakati mwamuzi Massimo Bussaca alimwonyesha kadi nyekundu kwa kufanya madhambi ndani ya 18 na kutoa penati ambayo Diego Forlan aliitumia kupachika goli la pili katika dakika ya 80.

KWa matokeo hayo, Afrika Kusini watatakiwa kuifunga Ufaransa katika mechi ya mwisho na Mexico itoke sare na Ufaransa kisha mechi ya mwisho Mexico iifunge Uruguay. Hayo ni mambo ya pata potea, lakini katika hali halisi itabidi Afrika Kusini wawe watazamaji baada ya hatua ya awali.

Kuona matokeo live na msimamo wa makundi unatakiwa kuwezesha javascript.

BBC navigation

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.