27 Juni, 2010 - Imetolewa 16:51 GMT

England yachapwa na Ujerumani 4-1

Miroslav Klose akipongezwa na wenzie baada ya kuandika goli la kwanza la Ujerumani.

Ujerumani imefuzu kucheza robo fainali ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini, baada ya kuifunga England mabao 4-1 katika uwanja wa Free State mjini Bloemfontein.

Mechi hiyo ambayo England walionyesha kulemewa katika safu ya ulinzi, pia itakumbukwa kwa kukataliwa bao la wazi lililofungwa katika dakika ya 38 na Frank Lampard.

Ujerumani walitangulia kufunga katika dakika ya 20 kupitia Miroslav Klose, na katika dakika ya 32 Lukas Podolski akaongeza goli la pili.

Katika dakika ya 37, England walipata kona na mlinzi Mathew Upson akafunga kwa kichwa kuipatia England goli pekee. Dakika moja tu baada ya bao hilo Frank Lampard alipiga mpira wa mbali ambao uligonga juu ya mwamba kabla ya kudunda ndani ya goli la Ujerumani.

Utata

Lakini mwamuzi Uruguay Jorge Larrionda kutoka Uruguay alifuata ushauri wa msaidizi wake wa pembeni na kuendeleza mchezo bila kutambua bao hilo.

Kipindi cha pili kilimalizika Ujerumani wakiongoza 2-1, na majaribio kadhaa ya mashambulizi ya England hayakufanikiwa.

Thomas Mueller alizamisha kabisa matumaini ya England kwa kufunga mabao mawili katika kipindi cha dakika tatu, moja katika dakika ya 67 na la nne katika dakika ya 70.

Kocha wa Ujerumani, Joachim Loew, akiwa ameshapata imani ya ushindi alifanya mabadiliko yaliyoonekana ya kuwapumzisha washambuliaji muhimu kwa ajili ya robo fainali.

Meneja wa England, Fabio Capello, pia alifanya mabadiliko kadhaa katika kipindi cha pili kuimarisha ushambuliaji lakini bila mafanikio.

Takwimu

Hapo chini ni jedwali linalokupa maelezo ya mechi kadri ilivyofanyika, utaweza kuona wachezaji walioanza na wa akiba, wafungaji na maelezo mengine kama kadi na umiliki wa mpira.

Kuona matokeo live na msimamo wa makundi unatakiwa kuwezesha javascript.

BBC navigation

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.