Filamu ya bin Laden marufuku Pakistan

Image caption Osama bin Laden amekuwa mafichoni kwa miaka mingi, akisakwa pamoja na sehemu nyingine Pakistan na Afghanistan.

Bodi inayosimamia filamu nchini Pakistan imepiga marufuku mchezo wa kuigiza ukimhusu Osama Bin Laden kuonyeshwa nchini humo. Mchezo huo uliopewa jina la Tere Bin Laden, filamu hiyo inasimulia visa vya mtu anayefanana na mtu anayetakikana kuliko wote duniani.

Kampuni kuu inayosambaza filamu hiyo imeiambia BBC kuwa imekata rufaa kupinga uamuzi huo. Bw Nadeem Mandviwala amesema kuwa kwa sasa amewasilisha hoja yake kwa Wizara ya utamaduni.

Kabla ya hapo, bodi inayosimamia filamu ilitaja sababu za kuizuia filamu hiyo isonyeshwe. Sababu kuu ilikuwa kumuonyesha Osama Bin Laden kama kichekesho. Sababu nyingine ni matumizi ya lugha isiyostahili, pamoja na kile kilichotajwa kama kudhalilisha vyombo vya sheria nchini humo katika filamu hiyo.

Ingawa hatua hii haikutarajiwa hakuna la kushangaza kutokana na kwamba serikali ya nchi haipendi kugusia wala kujihusisha na suala la Osama Bin Laden. Ingawa hajulikani alipo, maofisa wa Marekani wana imani kuwa bado yumo mafichoni nchini Pakistan.

Pamoja na hayo yote, Bw Mandviwala anasema kuwa ana imani kuwa kikwazo hicho kitaondolewa. Wizara ya utamaduni itatangaza uamuzi wake