Semenya ashinda mbio Finland

Image caption Caster Semenya ashinda mbio za Finland

Bingwa wa dunia wa mbio za mita 800 Caster Semenya ameshinda mbio zake za kwanza tangu kuruhusiwa kurudi kwenye mashindano baada ya kufanyiwa uchunguzi kuhusu jinsia yake.

Alimaliza mbio hizo kwenye mashindano ya Lappeenrata katika muda wa 2:4:22. Katika mbio za mwaka uliopita mjini Berlin alimaliza katika muda wa 1:55:45.Hajashiriki katika riadha kwa muda wa karibu mwaka mmoja na aliridhika kumaliza mbio za Finland katika muda huo.

''Nilikuwa na wasiwasi kwa sababu ni muda mrefu sijashindana. Ni mwanzo mpya.''

Semenya,ambaye atashiriki tena kwenye mbio za Jumapili za Lapinlahti, pia anatarajia kushiriki mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini Delhi,India. Huko huenda akakutana na mwanariadha wa Uingereza Jenny Meadows, aliyepata medali ya shaba katika mashindano ya mwaka uliopita mjini Berlin.