Arsenal yaibamiza Blackpool 6-0

Theo Walcott alifunga hat-trick (magoli matatu mechi moja) yake ya kwanza tangu aanze kucheza alipoisaidia Arsenal kupata ushindi wa magoli 6-0 dhidi ya Blackpool katika mechi waliyotawala kwenye uwanja wa Emirates mjini London.

Image caption Theo Walcott alikuwa mwiba kila alipokuwa na mpira kuwakabili walinzi wa Blackpool.

Blackpool waliopanda daraja msimu huu na ambao katika mechi ya ufunguzi waliichapa Wigan 4-0, walianza mechi hiyo vizuri, lakini Walcott alikuwa moto wa kuotea mbali wakati alipofunga goli la kuongoza.

Penati iliyopigwa na Arshavin iliipatia Arsenal goli la pili, pamoja na Ian Evatt kutolewa nje kwa kadi nyekundu, kabla ya Walcott kuongeza la tatu kunako dakika ya 39.

Abou Diaby alidokoa mpira ulioingia wavuni kwa ustadi, Walcott akafanya mambo kukamilisha hat-trick na Marouane Chamakh akafunga la sita kwa uhodari mkubwa kuandika la sita na la mwisho.

Baada ya kutoka sare na Liverpool 1-1 kwenye mechi ya kwanza, Gunners sasa wamepata ushindi wao wa kwanza. Arsene Wenger atakuwa amefurahi, lakini bado ana kazi ya kujenga ulinzi na kuongeza mlanda mlango mwingine.

Wafungaji:-

  • Walcott 12
  • Arshavin (pen) 32
  • Walcott 39
  • Diaby 49
  • Walcott 58
  • Chamakh 83

Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa Jumamosi, tarehe 21 Agosti 2010.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii