ANDRE AYEW

Andre
Image caption Andre 'Dede' Ayew

Andre Dede Ayew alivuka kwa haraka hadi jukwaa la kimataifa na hadhi ya juu japo haikuwa kwa urahisi.

Mchezaji huyo wa miaka ishirini na moja anatoka familia ya vigogo wa soka; babake Abedi Ayew Pele alikuwa mshindi mara tatu wa tuzo la mwanasoka bora Afrika na ami yake Kwame Ayew Pele amewahi kuchezea nchi yake Ghana, kimataifa na alishiriki mechi za Olimpiki za mwaka wa 92.

Bofya hapa kupiga kura:

Kutokana na historia kama hiyo imekuwa vigumu zaidi kwa Dede kujisimamia kidete na kujitengea wasifa wake katika soka kimataifa na ni hivi punde tu ameanza kushamiri.

Machachari yake katika mechi aliyochezea Ghana katika kombe la Dunia mwaka huu wa 2010 ndiyo yaliyomng'arisha zaidi.

Mrama

Mechi hiyo ilipamba sifa ya awali aliyopata katika mechi ya taifa bingwa barani aliyochezea Ghana 2010 na nyingine aliposhika unahodha wa timu ya kitaifa ya wachezaji wasiozidi miaka 21 na kunyakua kikombe.

Lakini mwaka mmoja tu kabla ya hapo, mambo yake yalikuwa mrama.

Alikuwa ameteuliwa na kocha mfaransa wa Ghana Claude Le Roy katika timu ya taifa katika kombe la taifa bingwa barani Afrika mwaka wa 2008, licha ya pingamizi nyingi na shutuma zilizmzidia alipozembea katika mechi hiyo.

Lakini amejikwamua kutoka giza hilo na kuonyesha kukomaa akiwa anachezea kwa mkopo Arles Avignon kabla ya kumshawishi kocha Didier Deschamps kumchukua kwa timu ya kwanza ya Marsille.

Kwa msimu huu pekee amejing'arisha katika timu hiyo ya ufaransa kwa kuwafungia mabao manne.

Tuzo ishirini na tisa kibindoni na yungali na umri mdogo wa miaka 29 tu bado ana mengi ya kufikia.

MAONI YA WATAALAMU JUU YA ANDRE AYEW

Iwapo kuna mchezaji aliyeonyesha ukakamavu na uvumilivu mkubwa basi ni Dede Ayew.

Image caption Andre Ayew

Kijana huyu hakuwahi kusikika miaka mitatu tu iliyopita alipokuwa akichezea timu ya taifa ya Ghana ya wachezaji wasiozidi miaka 17. Wengi walidhania kuwa anabembea kwa jina maarufu la familia yake kujipatia sifa kimataifa.

Wako wapi sasa hao waliomkashifu? Lakini naye pia alivyopanda hadhi katika timu za vijana machachari hadi kuingia timu za wachezaji wakubwa ndivyo alivyokomaa katika uchezaji wake na kuiwakilisha nchi yake kwa umahiri.

Image caption Ayew

Licha ya kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Ghana ya wachezaji wa chini ya miaka ishirini, alikuwa mchezaji muhimu sana katika mechi ya nusu fainali ya taifa bingwa barani Afrika nchini, ambapo alisaidi Ghana kufuzu kwa fainali kwa mara ya kwanza katika miongo miwili.

Licha ya kushindwa bao moja kwa nunge, na wasindi mara saba wa kombe hilo Misri, Black Stars hao walijisifia sana kwani hawakuwa na wachezaji wao wakuu Michael Essien, Stephen Appiah na Sulley Muntari.

Akiwa na miaka 21, mchezaji huyo alirejea katika jukwaa la kimataifa tena kwa kishindo baada ya kujipatia tuzo la mchezaji bora wa mechi mara mbili katika kombe la dunia nchini Afrika Kusini.

Pia aliteuliwa kwa tuzo la mchezaji bora zaidi mwenye umri mdogo katka mechi hiyo yote, japo alishindwa na Mjerumani Sami Khedira. Uchezaji wa Ayew umedhihirika wazi katika msimu huu kuwa wa hali ya juu zaidi nkuipa sifa nchi yake Ghana na kweli anastahili pongezi.