ASAMOAH GYAN

Bila ya shaka Asomoah Gyan ataridhika na jinsi alivyoshamiri mwaka huu ambapo aliiwakilisha Ghana katika mashindano makubwa mawili.

Image caption Asamoah Gyan

Mwaka ulianza kwa ishara nzuri wakati Gyan alipoisaidia nchi yake kufika kwenye fainali za mataifa ya bara Afrika ingawa walishindwa na Misri bao 1-0.

Kikosi cha Ghana kilikosa wachezaji mashuhuri kama vile Stephen Appiah, Sulley Muntari, John Mensah na Michael Essien wakati wa michuano hiyo iliyofanyika nchini Angola. Hivyo basi chipukizi wa Ghana walimtegemea sana Gyan kuwapa moyo.

Mabao matatu

Bofya hapa kupiga kura:

Gyan hakusita kuonyesha ustadi wake huku akifunga mabao matatu kati ya manne ambayo yaliisukuma Ghana hadi fainali kwa mara ya kwanza mnamo kipindi cha miaka 18.

Aliendelea na makali hayo hadi fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini ambapo pia alifunga jumla ya mabao matatu ambayo yaliipeleka Ghana hadi robo fainali.

Kutokana na ushari wake Gyan alikuwa mchezaji wa pili kutoka bara Afrika kufunga mabao mengi katika historia ya kombe la dunia.

Rekodi hiyo inashikiliwa na mshambuliaji wa zamani wa Cameroon, Roger Milla ambaye alifunga mabao manne.

Image caption Asamoah Gyan

Uhodari wake hawakuonekana tu alipokuwa akichezea timu ya taifa, Black Stars. Kwenye kilabu yake ya Rennes huko Ufaransa, Gyan alifunga mabao 13 ambayo yalikiwezesha kumaliza katika nafasi ya tisa ya ligi.

Alipohamia Sunderland mnamo mwezi wa Agosti alidhihirisha machachari yake kwa kufunga bao la kuvutia zaidi katika mechi yake ya kwanza katika ligi ya Uingereza. Sunderland walitoka sare 1-1 na Wigan.

Kadi nyekundu

Licha ya umaarufu huu, Gyan pia alikumbwa na dosari wakati alipokosa kufunga penalty ambayo ingeiwezesha siyo tu Ghana bali bara zima la Afrika kufika kwenye nusu fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

Pia alionyesha hasira zake kwa kumgonga mchezaji kutoka Sudan wakati wa mechi ya mchujo mwezi uliopita, kosa ambalo lilimfanya apewe kadi nyekundu.

Ingawa Gyan hajapa umaarufu mkubwa kimataifa, ametambuliwa na FIFA na kuteuliwa miongoni mwa wachezaji wengine 23 kuwania tuzo ya mchezaji bora zaidi duniani wa kandanda.

ASAMOAH GYAN

Image caption Mshambuliaji wa Ghana na Sunderland Asamoah Gyan

Ukizingatia jinsi alivyoichezea klabu yake pamoja na kuiwakilisha nchi yake mwaka wa 2010, ninaamini mwanasoka ambaye anastahili kupewa tuzo ya mshindi wa shindano la BBC la mchezaji bora zaidi barani Afrika si mwingine bali ni mshambuliaji wa Ghana Asamoah Gyan.

Mara kwa mara wale ambao huzingatiwa kwa tuzo kama hii huwa ni wale wanaochezea vilabu vikubwa vya Ulaya.

Kwa mantiki hiyo hapana shaka kwamba mshambulizi wa Chelsea Didier Drogba kutoka Ivory Coast au mchezaji wa Inter Milan, Samuel Eto’o kutoka Cameroon watakuwa kwenye mstari wa mbele kutokana na umaarufu wa vilabu hivyo.

Ubora

Lakini kiwango cha mchezo wao kilikuwa bora tu kwa vilabu vyao. Gyan mwenye umri wa miaka 25 alionyesha ubora wake kwa kuwa nguzo katika timu ya taifa Black Stars ambao walimaliza katika nafasi ya pili ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Alifunga mabao matatu kati ya manne ambayo yaliiwezesha Ghana kupiga hatua katika mashindano hayo yaliyofanyika jijini Angola mwezi Januari ambako walitandikwa 1-0 na Misri.

Image caption Asamoah Gyan

Miezi sita baadaye alionyesha uhodari wake kwenye fainali za kombe la dunia ambako Black Stars ilikuwa timu ya pekee kutoka Afrika kufika robo fainali.

Cameroon na Senegal ndiyo mataifa pekee ya Afrika ambayo yamewahi kuhitimu robo fainali ya mashindano ya kombe la dunia.

Itakumbukwa kwamba timu zote za Afrika ambazo zilikuwa na wachezaji wenye sifa kubwa kimataifa, zilitimuliwa mapema katika michuano hiyo ya fainali za Kombe la Dunia.

Hadi robo fainali, Gyan alikuwa ameipatia Black Stars jumla ya mabao matatu.

Image caption Asamoah Gyan

Huko Rennes, Ufaransa Gyan aliendelea kuonyesha ushari wake ambako alifunga mabao 13 na kujinyakulia nafasi ya tano kama mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye ligi kuu ya Ufaransa.

Ingawa Gyan hachezei kilabu maarufu sana barani Ulaya, FIFA wametambua jitihada zake na kumtaja miongoni mwa washindani 23 wa tuzo la mcheza kandanda bora zaidi duniani.

Wakati umewadia wakutawaza kuwa mfalme wa kandanda Afrika kutokana na jitihada zake ambazo zimeleta sifa kwa kilabu yake ya Ulaya, nchi yake na bara zima.