Hassan Ndayishimiye aandikisha historia kwa kuwa mchezaji wa kwanza wa tennis kutoka Burundi kucheza Wimbledon

Mchezaji tennis chipukizi kutoka Burundi, Hassan Ndayishimie, leo amefanikiwa kuandikisha historia kwa kuwa mchezaji wa kwanza kutoka taifa hilo kushiriki katika mashindano ya Wimbledon.

Lakini Ndayishimiye sio tu alionyesha nia ya kushiriki, bali aliweza pia kumshinda mpinzani wake Matias Sborowitz kutoka Uchina.,

Image caption Ameandikisha historia Wimbledon

Alipata ushindi wa 6-6 6-4.

Ndayishimiye alishiriki katika pambano la vijana wa umri mdogo la mchezaji mmoja kwa mmoja, yaani singles.

Kati ya mapambano mengine ambayo yalitazamiwa katika uwanja wa 17 wa Wimbledon ni pambano la mchezaji mwingine pia kutoka Afrika, Ons Jabeur, ambaye ni raia wa Tunisia, na aliyetazamiwa kucheza na Risa Ozaki kutoka Japan.