Tyson Gay kutoshiriki riadha mwaka huu

Image caption Mwanariadha Tyson Gay

Tyson Gay atakosa mashindano ya riadha ya Dunia baada ya kufahamika kuwa hatoshiriki kwenye riadha msimu mzima mwaka huu kutokana na jeraha la nyonga.

Gay mwenye umri wa miaka 28, ambaye angekuwa mmoja wa washindani wakuu wa Usain Bolt Korea Kusini,alijiondoa kabla ya kushiriki kwenye mchujo wa Marekani katika nusu fainali ya mbio za mita 100m.

Gay sasa ataangazia kujiandaa kwa Olimpiki mwaka ujao jijini London.

Mapema msimu huu alimaliza katika muda wa sekunde 9.79 mbio za mita 100m -ikiwa ni muda wa haraka zaidi duniani mwaka huu.

Katika mbio za mchujo nchini Marekani,Gay alikuwa amefuzu kwa muda wa sekunde 10.01,nyuma ya mwanariadha Ivory Williams,lakini akajiondoa kabla ya nusu fainali,akisema kuwa jeraha alilopata kwenye nyonga linamsumbua.