M-Australia kushinda Tour de France

Katika hatua ya mwisho kuhitimisha mbio za baiskeli za Ufaransa mwaka 2011 Cadel Evans akiwa ni raia wa Australia anasubiri tu wakati atangazwe kuwamshindi wa mbio za mwaka huu.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Cadel Evans kushinda Tour de France

Ikiwa Evans atashinda atakuwa raia wa Australia wa kwanza kushinda mbio hizi baada ya kuweka mda wa dakika 55 na sekunde 40 kunyakua shati la njano kutoka kwa Andy Shlek wakati baiskeli zikiingia hatua ya mwisho kuingia jiji la Paris leo.

Schleck kutoka Luxembourger alianza siku kwa kuongoza msafara lakini majaliwa yake kama msimu uliopita aitabidi aridhike kumaliza katika nafasi ya tatu..

Evans, aliyemaliza wa pili mwaka 2008 na 2009, alionyesha machozi ya furaha wakati akikabidhiwa jezi la njano.

Mwaka 2008 gwiji wa mashindano haya Alberto Contador alipokosa kushiriki, Raia huyu wa Australia alidhaniwa kushinda kwa urahisi lakini alishindwa na Carlos Sastre.

Kwa bahati nzuri mwaka huu amekabidhiwa jezo la njano ikiwa safari inakaribia mwiho katika mji wa Paris.

Mwenyewe Evans anasema kuwa ufanisi wake umetokana na juhudi pamoja na mipango ya mda mrefu na bahati ya kutofikwa na mikasa.

Mara ya mwisho kwa Evan kuvikwa jezi la njano ilikuwa kwenye hatua ya nane ya mashindano ya mwaka jana, lakini hakuweza kudhibiti nafasi yake akiongoza na hivyo kupitwa na Schlek walipofika sehemu za milima.

Lakini mara hii mashindano yalipofika kwenye tambarare Maustralia akatumia kipaji chake cha kasi na kulipiza kisasi.

Image caption Tour de France

Hivyo akaweza kunyoa pengo kubwa la sekunde 4 mda ambao ulimwezesha kumngoa kakake Schlek Frank kabla ya kuvuta kasi na kuweka rekodi ya sehemu hiyo ya mashindano kwa mda wa saa 2 na dakika 31.

Furaha ya kaka hao wawili ni kwamba watapata faraja ya kumaliza kwenye jukwaa wakiwa ndugu wa kwanza kusherehekea kwa pamoja kumaliza mashindano haya ya Tour de France.

Image caption Mark Cavendish

Muingereza Mark Cavendish anatazamia kua Muingereza wa kwanza kuvishwa jezi la kijani.

Hii ni kutokana na wingi wa pointi alizokusanya kufikia hatua ya mwisho ya mbio hizi baada ya kushinda hatua nne ya mashindano haya na hivyo kukusanya pointi 15.

Hata hivyo bado ana kibarua kukiwa na jumla ya pointi 65 hadi kuingia mjini Paris lakini Cavendish ameapa kujitolea kushinda hatua ya Champs Elysee kwa mara ya tatu na hivyo kujishindia jezi ya kijani.

Nyuma yake Cavendish ni Jose Joachin Rojas anayemfuata kwa karibu kabisa na ambaye anaweza kuharibu harusi ya Cavendish kwa kumpiku katika hatua hii ya mwisho hadi Paris.