Balotelli atolewa kwa 'mzaha' uwanjani

Mchezaji wa Manchester City Mario Balotelli alitolewa nje katika kipindi cha kwanza katika mechi yao dhidi ya LA Galaxy kwa kutoonyesha heshima kwa wapinzani wake.

Haki miliki ya picha bb
Image caption Mancini na Balotelli

Mshambulizi huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 20 alikuwa karibu kufunga goli,lakini hakufunga na badala yake akapiga mpira kwa kisigino na kukosa kufunga.

Kocha wa Manchester City Roberto Mancini alimpumzisha Balotelli kutokana na tukio hilo lakini wakati akitoka nje ya uwanja akajibizana na kocha wake.

Awali Balotelli alifunga bao kupitia mkwaju wa penalti katika mechi hio ya kirafiki ilomalizika kwa sare ya 1-1.

Man City Imepata ushindi wake wa tatu katika mechi zake za kujiandaa kwa msimu wa ligi kuu ya England.Katika uwanja huo mashabiki wa LA Galaxy walimzomea Balotteli kwa kitendo chake hicho.

Hii si mara ya kwanza kwa mchezaji huyo wa zamani wa Inter kujikuta katika matatizo na Kocha Mancini, ambaye pia alikuwa kocha wake nchini Italia.