Ferguson:Nimeridhika na wachezaji kwa sasa

Image caption Furguson ametosheka na wachezaji

Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson anasema hatomsajili mchezaji yoyote hadi pale watakapokabiliana na majirani zao Manchester City katika uwanja wa Wembley.

Tayari ameshamsajili Ashley Young, Phil Jones na mlinda mlango David de Gea.

Kiungo wa Inter Milan Wesley Sneijder amehusishwa na Manchester United.

Lakini Ferguson anasema: "kwa wakati huu,sioni nikongeza mchezaji mwengine. Mchezaji ambaye tunamuhitaji hatujamuona kwa sasa."

Aliongeza kuwa: " Tumepoteza wachezaji watano mwaka huu kutokana na wao kuwa na umri wa miaka thelathini na zaidi.

"Hilo limetusaidia kupata pesa za kuwasajili wachezaji watatu vijana niliowaleta kwenye timu.

"Nimeridhika na wachezaji nilionao kwa sasa."

Kutokana na kustaafu kwa kiungo Paul Scholes,majina kadhaa yametajwa kama yanayofikiriwa kujumuishwa kwenye kikosi cha Manchester United kama vile Sneijder, Samir Nasri wa Arsenal na Luka Modric wa Tottenham.

Hata hivyo Ferguson amekanusha kama anafikiria kumsajili Sneijder, akisema kwamba "hana nia ya kumsajili".