Man U v Liverpool kubwa kuliko Barca v Real

Fergie Haki miliki ya picha AP
Image caption Sir Alex Ferguson

Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema mchezo kati ya timu yake dhidi ya Liverpool ni mechi kubwa kubwa zaidi duniani katika ngazi ya vilabu.

Timu hizo mbili zinakutana kwenye uwanja wa Anfield siku ya Jumamosi na Ferguson anaamini mpambano huo unazidi hata mpambano wa vigogo wa Uhispania Barcelona na Real Madrid.

"Unajua tofauti ni - Barcelona iko upande mmoja wa nchi, na Madrid upande mwingine," alisema. "Mashabiki wa Huspania sio watu wa kusafiri.

"Mchezo pekee unaoweza kulinganishwa na United-Liverpool ni kati ya Rangers dhidi ya Celtis ya Scotland."

Ferguson ameongeza kusema: "Mimi huwa nauona ni kama mchezo mubwa wa msimu katika soka la England. Hii inahusisha historia ya vilabu vyote viwili na miji hiyo miwili."

Ferguson anakiri kuwa mechi kati ya Manchester United dhidi ya Manchester City huenda ukawa na msisimo wa aina yake katika miaka michache ijayo, lakini anaona mchezo dhidi ya Liverpool una hadhi yake.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mkali, lakini Ferguson amewataka mashabiki wa pande hizo mbili kuhakikisha kuna hali ya utulivu na kuheshimiana.

Alisema: "Uhasama kamwe hautabadilika, lakini nadhani pande hizo mili zinategemeana kisoka.