Wenger hana hofu mkataba wa Van Persie

Arsene Wenger Haki miliki ya picha AFP
Image caption Arsene Wenger

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema hana wasiwasi kwamba Robin van Persie si mwenye haraka ya kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo.

Nahodha wa Arsenal, ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2013, amesisitiza "nafsi yake imejitolea kwa klabu ya Arsenal".

Wenger amesema: "Iwapo utakuwa umejiwekea asilimia 100 hadi siku ya mwisho ya mkataba wako, hiyo yote naiita ni kujifunga kabisa.

"Kwangu mimi si suala kuwa na mkataba mrefu. Anafahamu tupo tayari kuzungumzia mkataba mpya.

Mshambuliaji huyo anayechezea pia timu ya taifa ya Uholanzi, ameainisha umuhimu wake kwa Arsenal kwa kupachika mabao mawili siku ya JUmapili, The Gunners walipoilaza Sunderland 2-1.

Van Persie, ambaye yumo katika kikosi cha Arsenal kwa karibu miaka saba, alitumia nafasi ya mkutano kabla ya mechi kutoa uhakikisho wake kwa mashabiki kwamba anafurahia kuendelea kuichezea klabu hiyo licha ya kutosaini mkataba mpya.

Amekuwa akihusishwa kujiunga na Manchester City, klabu ambayo iliwachukua Samir Nasri na Gael Clichy kutoka klabu hiyo ya London msimu huu.

Wenger ameongoza: "Jambo muhimu ni kile unachofanya uwanjani na namna unayojitolea kwa kadri utakavyobakia katika klabu.

"Suala muhimu ni kurefusha mkataba wake na iwapo hatafanya hivyo hamna budi kuheshimu hilo. Muhimu anacheza vile anavyopaswa kucheza.