Mancini apumua kwa ushindi wa "bahati"

Sergio Aguero Haki miliki ya picha PA
Image caption Sergio Aguero

Roberto Mancini amesema Manchester City walipata bahati baada ya bao la dakika za mwisho lililofungwa na Sergio Aguero na kuipatia timu yake ushindi wa mabao 2-1 dhdi ya Villarreal katika mchezo wa kundi A kuwania Ubingwa wa vilabu vya Ulaya.

Manchester City walionekana kupata shida ya kutoka bila ya ushindi katika mchezo wao huo wa tatu wa kundi lao la A hadi Aguerro aliyeingia akiwa mchezaji wa akiba na kufanikiwa kufunga bao la ushindi zikiwa zimesalia sekunde chache kabla mchezo huo kumalizika.

Mancini amesema: "Tulikuwa na bahati kwa sababu unahitaji bahati kufunga bao dakika za mwisho lakini hata hivyo tulistahili kushinda."

Manchester City wana michezo dhidi ya ugenini dhidi ya Villarreal na Napoli kabla haijaikaribisha Bayern Munich nyumbani.

Mancini anaamini mechi dhidi ya Napoli nchini kwake Italia itakuwa muhimu kwa timu yake kupata nafasi ya kusonga mbele katika kuwania Ubingwa wa Ulaya, ambapo City kwa sasa inashikilia nafasi ya tatu katika kundi la A nyuma ya Bayern Munich na Napoli.

Wachezaji wa Villarreal walilalamikia bao la ushindi la City baada ya mchezo kumalizika baada ya kupokonywa pointi moja.

Kocha wa Villarreal Juan Carlos Garrido amesema: "Wachezaji wake walidhani bao la ushindi la Manchester City lilikuwa la kuotea, lakini haikuwa hivyo. Lilikuwa bao la dakika ya mwisho na hakika inakuwa vigumu kumeza mate machungu."