India yaitandika England katika kriketi

England ilishindwa na India katika mfululizo wa mechi za siku moja za kriketi, baada ya kufungwa 3-0 na wenyeji katika mapambano ya mjini Mohali.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption India ikichezea nyumbani iliicharaza England 3-0

India ilipata ushindi wa wiketi tano.

India, ikijitahidi ifanikiwe kupta runs 299, ilianza vyema kupitia wachezaji Ajinkya Rahane, aliyefanikiwa kupata runs 91, lakini harakaharaka ilipoteza wiketi nne, lakini bado kufanikiwa kuonyesha ustadi mwishomwisho wa mchezo.

Mahendra Dhoni, pasipo kuondolewa, aliweza kuiletea timu yake ushindi kwa kupata runs 35.

Hapo awali, Jonathan Trott, bila kuondolewa, aliisaidia England kupata runs 98, na timu ikipata jumla ya runs 298.

Kevin Pietersen aliiwezesha England kupata 64, huku Samit Patel akizoa 70.