Chelsea nayo yaboronga kwa QPR

Faurlin Haki miliki ya picha Getty
Image caption Faurlin alikuwa mchezaji bora wa mchezo huo

Chelsea imebanwa na QPR na kuchapwa 1-0 katika mchezo uliojaa vuta nikuvute na kadi nyingi.

Bao hilo pekee la QPR limefungwa na Heidar Helgoson katika dakika ya 10 kwa mkwaju wa penati. Penati hiyo ilitokana na Helguson kusukumwa ndani ya boksi na David Luiz.

Jose Bosingwa alioneshwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Shaun Wrght Phillips, kabla ya Didier Drogba naye kutolewa uwanjani kwa kumchezea rafu Adel Taarabt.

Chelsea wangekwenda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo iwapo wangepata ushindi katika mchezo huu, kufuatia Man United kuchabangwa magoli 6-1 na Man City mapema.

Hata hivyo ushindi huu umeipeleka QPR hadi nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi kuu ya England.

Kwingineko Tottenham wakicheza ugenini wamewalaza Blackburn Rovers 2-1. Rafael Van der Vaart akifunga mabao yote ya Spurs. Bao pekee la Rovers lilifungwa na Mauro Formica.