Manchester United na Manchester City

Aliyekuwa mlinzi wa Manchester United Gary Pallister anaamini kwamba pambano la Jumapili dhidi ya Manchester City linachukua mahali pa mchuano na Liverpool kuwa ndio pambano lao la msimu.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Alisema mechi kali yao zaidi ilikuwa wikendi iliyopita dhidi ya Liverpool

Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson amesema pambano kati ya Man U na Liverpool ndio pambano kubwa kushinda yote kati ya vilabu vya kandanda duniani.

Lakini Pallister ameiambia BBC Sport: "City wamewakiuka United katika msimamo wa Premier League na wamethibitisha kwamba watakuwa wapinzani thabiti kwa ubingwa wa msimu huu.

"Hili huenda likawa ndilo pambano kubwa zaidi kwa United hata kushinda pambano na Liverpool."