Man U, Arsenal zasonga mbele Carling

Owen Haki miliki ya picha PA
Image caption Owen na Berbatov walitikisa nyavu

Manchester United imesonga mbele na kuingia katika 16 za mwisho baada ya kuizaba Aldershot 3-0 katika mchezo wa raundi ya nne wa Kombe la Carling.

Magoli ya United yalifungwa na Dimitar Berbatov, Michael Owen na Antonio Valencia.

Arsenal nayo imeichapa Bolton 2-1. Bolton ndio walikuwa wa kwanza kuliona lango la Gunners kupitia Fabrice Muamba.

Hata hivyo Arsenal walijibu mashambulizi na kupata bao la kusawazisha kupitia Andrey Arshavin, na goli la ushindi kufungwa na Park Chu Young.

Kwingineko Cardiff ilipata ushindi baada ya kuichapa Burnley 1-0.

Crystal Palace nayo ikaifunga Southampton 2-0.

Michezo mingine ya raundi ya nne itachezwa siku ya Jumatano, ambapo Stoke City itacheza na Liverpool, Wolverhampton kupambana na Manchester City, Blackburn kucheza na Newcastle, na Everton kuikaribisha Chelsea.