Tevez apewa adhabu ya kukatwa mshahara

Tevez Haki miliki ya picha Getty
Image caption Carlos Tevez kukatwa mshahara

Mshambuliaji wa Manchester City Carlos Tevez amepewa adhabu ya kukatwa mshahara wa wiki nne, na onyo la maandishi baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka mkataba wake.

Mchezaji huyo kutoka Argentina amepewa pia adhabu ya kutocheza soka kwa wiki mbili, lakini adhabu hiyo tayari amekwisha tumikia.

City imemkuta na hatia Tevez ya makosa matano, ikiwemo kugoma kupasha moto misuli katika mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich, Septemba 27.

Mchezaji huyo ana muda wa siku 14 iwapo anataka kukata rufaa.