Tevez sasa kukatwa mshahara wiki mbili

Manchester City imepunguza adhabu ya Carlos Tevez na sasa atakatwa mshahara wa wiki mbili baada ya Chama cha Wacheza kandanda ya Kulipwa (PFA) kugoma kuidhinisha adhabu ya kukatwa mshahara wa wiki nne.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Carlos Tevez

City ilimtia hatiani mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina kwa kukiuka vifungu vitano vya mkataba wake wakati wa mechi ya Ligi ya Ubingwa wa Ulaya mwezi wa Septemba dhidi ya Bayern Munich.

Lakini PFA ilinga mkono madai ya Tevez kwa kutaaa kupasha moto mwili na kusema faini anayostahili ni kukatwa mshahara wa wiki mbili tu kama inavyotakiwa.

City imeishutumu PFA kwa kuonesha "kugemea upande mmoja" wakati wa kushughulikia shauri hilo.

Taarifa ya Manchester City imesema: "Manchester City imevunjika moyo kutokana na PFA kuonesha upendeleo katika mchakato mzima wa kushughulikia suala hilo.

"Carlos Tevez binafsi aliwakilishwa muda wote na mtendaji mkuu wa PFA Gordon Taylor, ambapo klabu iliarifiwa tu kwamba PFA imefikia uamuzi.

"Manchester City imekuwa katika mazungumzo ya kina na PFA tangu tarehe 28 mwezi wa Septemba. Uamuzi wa leo wa PFA ni kuonesha wameitupa mkono klabu katika mazungumzo.

Taylor, ambaye amekanusha kuengemea upande mmoja, alitoa taarifa mapema siku ya Alhamisi ambapo PFA ilisisitiza "haki haikutendeka" kwa kumtoza faini ya mshahara wa wiki nne, ambao unakaribia kiasi cha paundi milioni 1.

"Maoni ya PFA yalizingatia ushahidi wote uliowasilishwa, kwamba Carlos Tevez kamwe hakugoma kuichezea klabu hiyo," taarifa ya PFA ilieleza.