Newcastle nambari tatu sasa!

Mabao matatu kutoka kwa mshambulizi matata Demba Ba kuliiwezesha Newcastle kuendeleza rekodi yake ya kutoshindwa katika ligi ya Premier ya Uingereza msimu huu.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Demba Ba baada ya kuifungia Newcastle bao

Ushindi huyo wa jumatatu usiku kumuipandisha Newcastle hadi nafasi ya tatu wakiwa na jumla ya alama 22 baada ya kucheza mara kumi. Chalsea ambayo mwishoni mwa juma walifungwa na Arsenal mabao 5-3 wameshuka hadi nafasi ya nne.

Demba Ba ambaye ni mshambulizi wa timu ya Taifa ya Senegal alifunga bao la kwanza katika dakika ya 12 baada ya kupata pasi safi kutoka kwa Gabriel Obertan. Na kukiwa kumesalia dakika tano tu kipindi cha pili kumalizika ,Ba alifanya mambo kuwa 2-0.

Hata hivyo nusura Ba aharibu siku yake pale alipoisababishia Newcastle kuadhibiwa kwa mkwaju wa penalti baada ya kumsukuma Peter Crouch katika eneo la hatari.

Lakini Ba aliongoza bao la tatu katika dakika ya 81 nae kwa njia ya penalti.