Chelsea yatoka sare na Genk

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kocha Andre Villas-Boas ampa vidokezo Lampard

Chalsea imeendeleza hali yake ya kutofanya vizuri katika ligi ya Premier hadi katika mechi za Klabu bingwa bara Ulaya baada ya kutoka sare ya 1-1 na Racing Genk ya Ubelgiji katika mechi iliyochezwa Jumanne usiku.

Mshambulizi wa Brazil Ramires aliifungia Chalsea bao katika dakika ya 25 baada ya mchezo msafi kati yake , Fernando Torres na Raul Meireles.

Chalsea walikuwa na nafasi nzuri ya kufanya mabao kuwa 2-0 kabla ya kwenda mapumziko lakini mkwaju wao wa penalti uliopigwa na David Luiz uliokolewa kirahisi na kipa wa Genk.

Miamba wa Chalsea walitiwa adabu na Jelle Vossen huku Frank Lampard na Florent Malouda wakikosa nafasi kadhaa za kufunga.

Chalsea ilikuwa inacheza mechi hii ikikumbuka kichapo walichopewa na timu mpya ya katika ligi ya Premier ,Qeens Park Rangers na kisha kufuatia kunyolewa vibaya na vijana wa Arsenal.

Mkufunzi wao Andre Villas-Boas anasema hii ni wiki ya mkosi kwa Chalsea.

Katika kundi hilo hilo la E Bayer Leverkusen ya Ujerumani ilicharazwa 3-1 na Velencia ya Uhispania .

Licha ya kutoka sare, Chalsea bado inaongoza kundi E na alama nane,Ikifuatwa na Bayer Liverkusen wakiwa na alama sita. Genk ni ya mwisho na alama mbili.