Man U wacheza vibaya, lakini washinda.

Manchester United waliwafunga Otelul Galati mbili sufuri lakini walitolewa jasho na timu hiyo ya Rumania.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Antonio Valencia aifungia Man U bao la kwanza

Wakati Antonio Valencia alipoifungia Man U bao la kwanza katika dakika ya nane , mashabiki wa mashetani wekundi walikuwa na matumaini makubwa kuwa timu ya Otelul ingelibebeshwa gunia la mabao. kumbe sivyo!

Baada ya bao lao la kwanza, vijana Sir Alex Ferguson ambao walikuwa wanacheza nyumbani Old Traford hawakuwa na mchezo wa kuvutia.

Ni baadae sana katika dakika ya 87 ambapo Wayne Rooney aliifungia Manchester United bao la pili.

Hii ilikuwa ni mara yakwanza kwa Man U kucheza katika uwanja wao wa nyumbani tangu walipopigwa 6-1 na jirani zao Man City.

Tangu kipigo hicho Manchester United hawaja weza kutulia na kuonyesha mchezo wa kuvutia. Hata hivyo la muhimu nikuwa Jumatano usiku waliifunga Otelul Galati, 2-0 na kuzoa pointi tatu.

Baada ya matokeo ya mechi hizo Manchester sasa wanaongoza kundi C na point nane sawa na Benfica ya Ureno lakini kwa wingi wa magoli.