Ferguson asherehekea miaka 25 Man U

Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson anasherehekea miaka 25 na timu hiyo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sir Alex Ferguson asherehekea miaka 25 Man United

Ferguson ameeleza miaka hiyo 25 akiwa na mashetani wekundu ni kama hadithi nzuri.

Katika miaka hiyo yote mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 70 ameisaidia Man U kushinda kombe la Premier mara 12, kombe la FA mara tano na Ligi ya mabingwa bara Ulaya mara mbili.

Licha ya mafanikio hayo, Ferguson amekwa hapendelei sana kuzungumzia sifa hizo.

Na hata anapoulizwa kuhusu mafanikio yake Man United , Meneja huyo huanza na usemi wake wa kawaida " Sitazungumzia swala hilo".

Lakini mwaka jana akiwa na umri wa miaka 69 alizungumzia kwa muda enzi zake na mafanikio yake tangu alipochukuo uongozi wa Man U Novemba 6 mwaka 1986 kutoka kwa Ron Atkinson.

Kutoka mwaka huo Ferguson amenyakuwa mataji 27 na kushuhudia miamba wengi wakikuza vipaji vyao wakiwa klabu cha Man United.

Kwa wakati huu litakalongaliwa ni muda gani Fergerson atabakia kuwa kileleni mwa timu hiyo, swali ambalo amenukuliwa akijibu kwa kusema " ataendelea ilimradi afya yake inamruhusu kufanya hivyo"