Blatter aomba msamaha kwa matamshi

Rais wa Shirikisho linalotawala kandanda duniani, Sepp Blatter ameiambia BBC kua anaomba radhi kwa matamshi yake kuhusu ubaguzi wa rangi ambayo yalizua hisia.

Matamshi ya kiongozi huyo wa Fifa mnamo siku ya jumatano yalisikika kama yaliyokusudia kuchochea ubagusi wa rangi kwa kusema kua yangeweza kutatuliwa kwa kupeana mikono kufuatia matusi.

Bw.Blatter mwenye umri wa miaka 75 amesema katika mahijiano na BBC kua ''Linauma na bado nahisi maumivu kwa sababu sikuweza kuona kua haya yatatokea.

Unapokosea kwa kutamka neno ambalo si sahihi, naweza tu kusema, nakiri kosa langu kwa watu wote ambao niliwaudhi kwa matamshi yangu.''

Blatter amesisitiza kua ''mapambano yake dhidi ya ubaguzi wa rangi yataendelea'' na kwamba hatojiuzulu, ingawa vyombo vingi vya habari hususan vya Uingereza, wachezaji mpira, Mameneja, viongozi na wanasiasa wamemtaka ajiuzulu.

Sitojiuzulu, aliiambia BBC katika mahojiano ya kina na mhariri wa ichezo wa BBC David Bond, akiongezea suali, kwanini nijiuzulu?

"unapokabiliwa na tatizo sharti ukabiliane nalo. Sioni kama ni vyema kujiondoa kwa sababu hilo haliambatani na moyo na msimamo wangu wa kupambana na matatizo, hiyo ndio hulka yangu.

Blatter aliongezea kua mchezaji yeyote atakayepatikana na hatia ya ubaguzi wa rangu uwanjani yafaa atupwe nje ya mechi.

"mpango wa kutostahmili ubaguzi," alisema Blatter. "hili limekua funzo kubwa kwangu."

Matamshi ya Blatter aliyoyatoa mapema wiki hii, yalizusha taharuki na mshangao mkubwa nchini Uingereza.