Man U yakabwa na Newcastle

Ba Haki miliki ya picha PA
Image caption Demba Ba alifunga bao muhimu la penati

Manchester United imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Newcastle United.

Sare hiyo imeifanya Newcastle iliyo katika nafasi ya tatu kuwa pointi moja tu nyuma ya United iliyo nafasi yapili nyuma ya United.

Goli la Manchester United limefungwa na Javier Hernandez, huku goli ya Newcastle likifungwa na Demba Ba kwa mkwaju wa penati.

Kwingineko Tottenham imeizaba West Brom 3-1. Emmanuel Adebayor akifunga mabao mawili na moja likifungwa na Jermaine Defoe. Bao pekee la West Brom lilifungwa na Youssoufou Mulumbu.

Tottenham sasa wamejikita katika nafasi ya nne pointi moja nyuma ya Newcastle.

Chelsea nayo ilizinduka na kuizaba Wolves kwa magoli 3-0. John Terry, Daniel Sturridge na Juan Mata wakipachika mabao hayo.

Katika matokeo mengine Sunderland ikicheza nyumbani ilichapwa na Wigan 2-1, Everton nayo ikicheza ugenini iliizaba Bolton 2-0, Norwich kushinda 2-1 dhidi ya QPR na mchezo wa awali ulimalizika kwa Stoke City kuizaba Blackburn Rovers 3-1.