Huwezi kusikiliza tena

Burundi kuraruana na Sudan

Image caption Mabingwa watetezi Kilimanjaro kucheza robo fainali Jumanne

Michuano ya soka ya mataifa ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama CECAFA, inaendelea tena siku ya Jumatatu mjini Dar es Salaam, Tanzania, baada ya hatua ya makundi kukamilika siku ya Jumamosi.

Tayari timu 8 zilizoingia robo fainali zimeshajulikana, na Jumatatu mechi ya kwanza itakuwa ni kati ya Burundi itakayopambana na Sudan, na baadaye Zanzibar (Zanzibar Heroes) ikikabiliana na Rwanda.

Siku ya Jumanne Uganda itacheza na Zimbabwe, na baadaye mabingwa watetezi, Tanzania, kupambana na Malawi.