Shay Given kutocheza soka mwezi mmoja

Mlinda mlango wa Aston Villa Shay Given ameonekana hataweza kucheza kandanda kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kuumia msuli wa paja wakati walipofungwa na Manchester United 1-0.

Haki miliki ya picha 1
Image caption Shay Given aumia msuli wa paja na kutocheza mmojakwa mwezi

Given, aliumia kidogo msuli wa mguu wake wa kushoto kabla ya mapumziko.

Meneja wa Aston Villa Alex McLeish alisema: "Inasikitisha kumkosa Shay katika hali kama hiyo, kwa bahati mbaya haya hutokea katika mchezo wa kandanda."

Kiungo Jermaine Jenas naye aliumia kifundo cha mguu katika mechi hiyo hiyo dhidi ya Manchester United huku klabu yake ikisubiri matokeo ya uchunguzi.

Given ambaye pia ni mlinda mlango wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland, tangu alipojiunga na Aston Villa akitokea Manchester City msimu huu kwa kitita ambacho hajafahamika, ameshacheza mechi zote za Ligi Kuu ya England.

Mmarekani Brad Guzan, aliyechukua nafasi ya Given zikiwa zimesalia dakika saba kabla ya mapumziko walipolazwa na Manchester United, ataendelea kudaka wakati huu Given akiuguza jeraha lake.

McLeish ameongeza: "Hatuna budi kukabiliana na changamoto hizi na tutazikabili.