Redknapp asema Gareth Bale ana kila kitu

Gareth Bale asifiwa na mejena wake kwamba hana udhaifu Haki miliki ya picha AFP
Image caption Gareth Bale asifiwa na mejena wake kwamba hana udhaifu

Meneja wa klabu ya Tottenham Harry Redknapp amemsifia Gareth Bale kuwa ni mchezaji asiye na "udhaifu wakati wa uchezaji wake".

Bale alifunga mara mbili wakati Tottenham ilipoilaza Norwich kwa mabao 2-0 na kuweka rekodi ya ushindi wa nane katika mechi kumi za Ligi Kuu ya England.

Redknapp amesisitiza ni vilabu tajiri tu duniani ndio vinaweza kumnyakuwa mshambuliaji huyo lakini akaweka sawa Bale hauzwi

"Amejigamba: Ni vilabu kama Barcelona, Man City au Real Madrid ambao wanaubavu wa kulipa gharama za kumsajili."

Redknapp hakusita kuonesha namna anavyomhusudu Gareth Bale ambaye ana umri wa miaka 22, na hadi sasa ameshapachika mabao manane msimu huu kwa klabu yake ya Tottenham pia mabao matatu kwa timu yake ya taifa ya Welsh.

Meneja huyo wa Tottenham ameongeza: "Ni mchezaji wa ajabu sana. Ana kila kitu, sioni udhaifu wowote katika uchezaji wake.

"Anaweza kufunga kwa kichwa, ana nguvu kama dume la ng'ombe, ana mbio sana, chenga na mikwaju mikali. Na muhimu zaidi ya yote ni kijana mwerevu."

Bale alijiunga na Tottenham akitokea Southampton mwaka 2007 kwa kitita cha paundi milioni 7 lakini bei yake kwa sasa imepanda sana kutokana na kuimarika kwa kiwango chake kwa siku za hivi karibuni katika Ligi na pia mashindano ya Ulaya.

Mwezi Oktoba mwaka 2010 alipofunga mabao matatu pekee dhidi ya Inter Milan kwenye michuano ya Ubingwa wa Ulaya, dunia ilianza kumkodolea macho, lakini Redknapp amebainisha iwapo timu yoyote ya England au kutoka nje itapigwa chini.

Tottenham ipo nyuma kwa pointi saba dhdi ya vinara wa ligi Manchester City, huku wakiwa na mechi moja mkononi na wameipiku Chelsea inayoshikilia nafasi ya nne kwa pointi nne pia wakiwa na mechi moja mkononi.