Arsenal yasonga mbele kombe la FA

Henry Haki miliki ya picha PA
Image caption Henry arejea kwa kishindo

Thierry Henry amerejea Arsenal kwa kishindo na kuisaidia timu hiyo kusonga mbele katika michuano ya Kombe la FA baada ya kufunga bao pekee katika mchezo dhidi ya Leeds United.

Arsenal wamesonga mbele baada ya kupata ushindi wa bao 1-0.

Henry, 34, alifunga goli lake la 227 kwa Arsenal baada ya kurejea kuichezea klabu hiyo kwa mkopo wa miezi miwili.

Arsenal sasa itakutana na Aston Villa katika raundi ya nne ya kombe la FA katika mchezo utakaochezwa Januari 28.