Man.city yazipi kupaa

Kwa mara nyingine mshambuliaji Mario Balotelli alijitokeza kua kiini cha mgogoro na sababu ya kuipatia Manchester city ushindi ikipiga hatua dhidi ya mshindani wake wa karibu Manchester United.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Balotelli

Balotelli aliingia wakati Manchester City ikisukumwa na Tottenham 2-2 baada ya kurudisha mabao mawili katika kipindi kifupi ikionekana kuondoka na angalau pointi moja.

Wakati ikionekana kua Manchester City imepungukiwa na maarifa Bario Balotelli aliangushwa ndani ya eneo la hatari na beki Ledley King na mshambuliaji huyo kufunga bao la City na kuiweka Spurs nyuma ya viongozi wa Ligi kwa tofauti ya pointi nane.

Habari kubwa kutoka mchuano huo hata hivyo haukua ushindi wa City bali gumzo lilizunguuka jinsi Balotelli alivyomkanyaga kichwani Scott Parker.

Harry Redknap aliwambia wandishi habari kua alishangazwa na jinsi refa alivyoshindwa kuliona kosa la Balotelli akimkanyaga Parker makusudi. Hivyo, Balotelli akaongezea umaarufu wake kwa mashabiki wa klabu yake wanaompenda licha ya wengi kuhusu ni juha katika soka ya England.