Khan kuzichapa tena na Lamont

Peterson Haki miliki ya picha AP
Image caption Peterson atalazimika kupanda tena ulingoni

Mpambano kati ya Amir Khan na Lamont Peterson umethibitishwa na Chama cha Ngumi cha Dunia, WBA, kwa mujibu wa promota wa Khan.

Richard Schaefer amesema amepokea barua kutoka kwa WBA ikimjulisha kuhusu "uamuzi wao rasmi wa kuwepo na mpambano wa marudio mapema iwezekanavyo."

Khan alipoteza mikanda yake ya WBA na IBF kwa Peterson mwezi Disemba na alihoji vigezo kadhaa vilivyotumika katika mpambano huo.

Lakini Peterson anaweza kuuacha mkanda wa WBA kwa kuamua kutopigana.

Schaefer, ambaye ni mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Golden Boys ya promosheni alikiambia kituo cha michezo cha ESPN: "Nimefurahi amepata mpambano wa marudiano, nina imani tutaanza majadiliano na kufanikisha pambano hilo.

"Amir na Lamont ni vijana wazuri na wanamichezo mahiri ambao walipigana kwa dhati mjini Washington mwezi Disemba, na nina uhakika uamuzi huu utafirahiwa na mashabiki wa ndondi duniani kote."