Siri ya ushindi wa wanariadha wa Afrika

Macau
Image caption Patric Macau wa Kenya katika mbio za Berlin

Ukiandika katika wavuti wa tafuta wa Google "East African running" yaani "Wakimbiaji wa Afrika Mashariki" utapata taarifa nyingi zinazouliza kitu gani hasa kinawafanya wakimbiaji kutoka huko kuwa na kasi ya ajabu.

Kila mtu anatafuta siri ya ushindi, kwa hiyo watu wanasaka kujua sababu, lakini kuna jibu moja jepesi, na haya ni maoni yangu.

Katika riadha, watu wengu wanahusisha Afrika Mashariki na wakimbiaji wa mbio ndefu kutoka Kenya na Ethiopia.

Cha kuvutia hapa, wengi wa wanariadha hawa wanatoka katika maeneo matatu yenye milima kando ya Bonde la Ufa: Eneo la Nandi nchini Kenya, ambalo limepata mafanikio makubwa, na Arsi na Shewa nchini Ethiopia.

Baadhi ya watu wanasema kwa kuwa wakimbiaji hawa wanaishi na kufanya mazoezi katika maeneo yenye miinuko, wana nafasi nzuri ya kuwa wanariadha bora. "Wenyeji wa kwenye miinuko", na mazoezi magumu kumeongeza chembe chembe nyekundu za damu, kitu ambacho ni moja ya sababu ya mafanikio yao katika mbio ngumu. Hata hivyo, wanasayansi wanataja kuwa kama kuishi katika urefu wa zaidi ya mita 2000, kuna watu pia wanaishi katika miinuko kama hiyo nchini Mexico, Andes na maeneo mengi tu ya Asia ya Kati.

Kwa hiyo, kwa nini kundi la wakimbiaji wazuri wanapatikana katika maeneo hayo matatu tu?

Kwangu mimi, hapa ndipo naona historia ikichukua nafasi yake. Kitabu kilichopata tuzo nyingi cha Bale na Sang kuhusu wakimbiaji wa Kenya, kinaelezea nafasi ya wamisionari na wanajeshi wa Uingereza walivyosaidia katika wanariadha wa sasa.

Mara tu ukimbiaji rasmi ulipoota mizizi na mafanikio kuanza kuonekana, utamaduni wa kukimbia mbio ndefu ukaanza kujichochea. Hii ndio sababu, nadhani, Afrika Mashariki imekuwa na utamaduni wa kukimbia, na Mexici hawana uwezo huo.

Je kuna sababu za kibaiolojia?

Image caption Haile Gabre Selassie, mmoja wa wakimbiaji hodari wa Ethiopia

Kuna vielelezo viwili hapa na ni chakula na/au wana nasaba "maalum". Hatuhitaji kupoteza wakati mwingi kufikiria kuhusu chakula. Ndio, chakula bora kinahitajika kwa ajili ya mazoezi magumu, lakini hilo ni jambo la kawaida.

Jenetiki zimekuwa zikitazamwa zaidi na watafiti. Baadhi wamependekeza kuwa nasaba wa watu wa Afrika Mashariki zina uwezo wa kukabiliana na shuruba nzito, lakini utafiti mwingi umefikia jibu lile lile, kuwa kwa sasa, hakuna ushahidi wa hilo.

Katika utafiti wangu, nimeona huenda miili midogo na mepesi ya wakimbiaji kutoka Afrika Mshariki hueda ikawa sababu muhimu.

Baadhi ya taarifa zinaeleza jinsi walivyo na uwezo mkubwa wakimbiaji hawa na kufananishwa na jinsi mabondia wanavyofanya au waendesha baiskeli katika mbio maarufu za Tour de France, kupunguza uzito kwa makusudi kabla ya kushindana.

Pia ni vizuri kuwa na mwili mdogo na mwepesi katika hali ya joto kwa kuwa mwili hupunguza joto kirahisi - ukitazama viwanja vingi wa Olimpiki vina joto sana (kwa mfano, Beijing, Sydney, Atlanta, barcelona, Seoul, nk.).

Neno "kukimbia kiuchumi" limekuwa likitumika katika kufanyia utafiti kuhusu matumizi wa nguvu kidogo kwa wakimbiaji kutoka Afrika Mashariki ikilinganishwa na wazungu.

Sababu kuu ambayo watafiti wanasema ni kuwa kuwa na uzito mdogo katika miguu na vigingi kwa miguu (jambo ambalo ni kawaida kwa miili ya wakimbiaji wengi wa Afrika Mashariki) inamaanisha wakimbiaji hawa wanahitaji nguvu kidogo kushikilia mwendo wa kasi.

Hoja hii inaleta maana zaidi, kama ambavyo taarifa kuhusu ubora na sio mazoezi mengi wanayofanya. Mazoezi magumu na yanayosababisha moyo kwenda kasi yameripotiwa kufanywa, jambo ambalo ni tofauti na wale wa nchi nyingine. Kwa hiyo wakimbiaji hawa hujituma zaidi na kufanya mazoezi kwa njia tofauti.

Kwa kuongeza hilo, wakimbiaji wengi maarufu (asilimia 50-70) wanakuwa wamekimbia mbio ndefu tangu utotoni wakati wakienda shule: jambo ambalo ni msingi mzuri katika kufanya mazoezi magumu wakikua.

Makala hii imeandikwa na Ben Oakley, Mkuu wa idara ya Michezo na ukakamavu, Chuo Kikuu Huria.