Senegal yabanduliwa

Image caption Kily alifunga Equitorial Guinea goli la kihistoria

Wenyeji wenza Equatorial Guinea imeshangaza wengi kwa kuibandua njee ya mashindano ya kombe la nchi bingwa barani Africa .

Kabla ya mashindano hayo kuanza , Senegal ni mojawapo ya nchi ambazo zilikuwa zimepigiwa upato wa kushinda kombe hilo.

Lakini Equatorial Guinea ambayo katika nafasi ya 151 katika orodha ya FIFA ya hivi karibuni waliyakatiza mautumaini ya Senegal.

Aliyefungua ukurasa wa magoli ni Randy lakini katika dakika ya 89 Moussa Sow aliifngia Senegal bao na kufanya mambo kuwa 1-1.

Ni katika dakika za majeruhi ambapo mchezaji Kily alifumua mkwaju mkali toka umbali wa yadi 25 hadi kimyani. Hivi mambo ya kawa Equitorial Guinea 2 Senegal 1.

Japo matokeo hayo ni pigo kwa Senegal lakini ni furaha kwa timu ya Newcastle ya Uingereza kwani washambulizi wake Demba Ba na Papiss Cisse wanarudi uingereza kuisaidia timu yao katika mechi za Premier.